Friday, October 12, 2012

CAS TEGETA KIBAONI

Makamu Mwenyekiti Miss. Candida felix Shirima akiwa na Mchungaji wake Rev. RAPHAEL MWASILE kwa furaha na shangwe nyingi siku hiyo wakiawa katika siku yao maalumu  kabisa ya tarehe 07/10/2012 akimpa mkono wa kheri na baraka na pongezi Mchungaji wa kanisani hapo.
CAS TEGETA KIBAONI

vijana hao kwa furaha na shangwe wakiwa ndani ya sare zao safi kabisa katika kusoma shairi lililoandaliwa na mtunzi wao mahili NEEMA MSUTA.
 
CAS TEGETA KIBAONI

kijana anayejulikana kwa jina la Mathias Mkweji akiwa mstari wa mbele kabisa kumpa Mchungaji wake (Raphael Mwasile) mkono wa kheri na baraka kwa kazi anayoifanya kanisani hapo katika sikukuu yao Tarehe 7/10/2012.
CAS TAG TEGETA KIBAONI

Katika sikuu ya vijana kanisani hapo Bethany temple tegeta kibaoni vijana wakiwa katika maandalizi ya kuingia ndani ya ukumbi wa kanisa na kuanza sherehe yao kama ilivyo andaliwa..
mbele kushoto ni kijana Michael Sungura. 
kulia ni Binti anaejulikana kwa jina la Zuriet..

Wednesday, October 10, 2012

CA'S TEGETA KIBAONI

katika siku kuuu ya vijana iliyoadhimishwa kanisani hapo siku ya tarehe 0710/2012 kitaifa,katika kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG Tegeta kibaoni(Bethany Temple).




Wednesday, June 27, 2012

Rev: Raphael Mwasile

Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo akiwa pamoja na mke wake QUEEN MWASILE.

Tuesday, June 26, 2012

Mchungaji kiongozi: Raphael Mwasile 

Kwa furaha akisalimiana na mzee wa kanisa mahali hapo  Mr. FRANK MTYAMA mara baada ya kumaliza ibada kanisani hapo siku ya jumapili.


katikati ni mtoto anayeitwa kwa jina la Ester msuta.
katika sikukuu yao ya watoto inayofanyika kila mwaka kanisani hapo.

Ester ni mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kwa sasa na anaishi makumbusho kwa wazazi wake. Mungu amempa uwezo wa kushika maneno yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu na ndio hapo mtoto huyo akiwa anazungumza maneno hayo mbele kabisa ya umati mkubwa wa kanisa mahali hapo anapo abudu.
mstari wake unatoka katika yoh 11:3-5

Watoto kanisani hapo huwa wanaungana na watoto wenzao katika kuadhimisha sikukuu yao iliyopangwa kitaifa  chini ya uangalizi wa kanisa la Tanzania Assemblies Of God.kulia nini  mwalimu wao wa watoto ambaye pia ni Mama Mchungaji wa kanisa hapo. Mama huyo amekuwa na huduma ya watoto pamoja na huduma ya wamama kwa namna moja ama nyingine Mungu amempa karama mbalimbali kuweza kuzungumza na watu wa kila rika hasa wamama wenzake pamoja na watoto pia hata mabinti wengi wamekuwa wakipata faida nyingi kutokana na uwepo wa mama mchungaji huyo.






Monday, June 25, 2012

Ibada ya jumapili ya tarehe 24 june,2012


Mwimbaji wa Nyimbo za Injili
David Prosper: song mtazame yesu

Mzee wa kanisa na Mwimbaji wa nyimbo za injili  Mr. David Prosper kuagwa rasmi kwa ajili ya kwenda kuanza huduma ya kichungaji huko mkoani kilimanjaro,.
wakati Mchungaji kiongozi alipo kuwa akimuaga Mtumishi wa Mungu huyo alikuwa akiwa ni mtu mwenye furaha sana na huku akisema ya kwamba labda Mtumishi wa Mungu huyo Mr. David Prosper anaenda huko kwa ajili ya kumsaplies Mchungaji huyo hapo wakati atakapo kuja akiwa ameambatana na mke wake  na huku mkononi akiwa na cheti cha ndoa.

Mambo hayo yalitokea kwani walikuwa wamekaa kwa mda mrefu sana na Ndugu huyo Mr. David Prosper akiwa hajapata msaidizi kwa maana ya mke.