katikati ni mtoto anayeitwa kwa jina la Ester msuta.
katika sikukuu yao ya watoto inayofanyika kila mwaka kanisani hapo.
Ester ni mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kwa sasa na anaishi makumbusho kwa wazazi wake. Mungu amempa uwezo wa kushika maneno yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu na ndio hapo mtoto huyo akiwa anazungumza maneno hayo mbele kabisa ya umati mkubwa wa kanisa mahali hapo anapo abudu.
mstari wake unatoka katika yoh 11:3-5
Watoto kanisani hapo huwa wanaungana na watoto wenzao katika kuadhimisha sikukuu yao iliyopangwa kitaifa chini ya uangalizi wa kanisa la Tanzania Assemblies Of God.kulia nini mwalimu wao wa watoto ambaye pia ni Mama Mchungaji wa kanisa hapo. Mama huyo amekuwa na huduma ya watoto pamoja na huduma ya wamama kwa namna moja ama nyingine Mungu amempa karama mbalimbali kuweza kuzungumza na watu wa kila rika hasa wamama wenzake pamoja na watoto pia hata mabinti wengi wamekuwa wakipata faida nyingi kutokana na uwepo wa mama mchungaji huyo.